MAMBO MATANO YATAKAYOKUSADIA KUDEAL NA MPENZI WAKO MWENYE WIVU.

Kama upo kwenye mahusiano na mtu ambaye ana wivu balaa na kuonekana anataka kujua kila kitu na wakati mwingine unajihisi anakucontroll, basi fanya haya mambo ambayo yatamfanya asiwe anakusumbua kila mara kwa kukuliza uliza maswali.

Mshirikishe kwenye ratiba zako


Kitu kimoja ambacho kitakusaidia kudeal na wivu wa mpenzi wako ni kuwa pamoja kwa mda mwingi na kufanya mambo ya kila siku ya kawaida pamoja. Muonyeshe kuwa hamna mwingine ila ni yeye tu ambaye umevutiwa nae na unampenda. Amini ataona kuwa hauko bize sana kuangalia watu wengine na anaruhusiwa kujua kitu unachofanya. Kama unaenda shopping kariakoo au manzese muuulize siku moja kabla kama atataka kwenda na wewe. Hii itaonyesha kuwa ni kweli unaenda shopping na sio kwenda kumuona mtu mwingine. Wakati mwingine anaweza kukataa ila atajisikia huru kujua kuwa kila kitu kipo sawa



Wajulishe wengine kuwa upo kwenye mahusiano.


Mruhusu mpenzi wako awe sehemu ya maisha yako. Mtambulishe kwenye familia yako au marafiki zako, mpeleke kwenye party zako za kikazi na umtambulishe kwa wafanya kazi wenzako. Usiogope kutumia mda wako na rafiki zako, kirahisi tu nenda kwa marafiki zako na mpenzi wako. Kama ukimuacha na kukazana kuongea na marafiki zako, hii itamfamya awe na wivu zaidi.

Mpigie Simu Mara Kwa mara.

Watu wengine wanachukia sana wakiwa wanasumbuliwa kwa kupigiwa simu mara kwa mara iwe kwa kupigiwa simu au sms. Ila hii sio kwa wale wenye wivu. Kama mpenzi wako anapenda kujua kila kitu kuhusu wewe, na ukagundua hilo basi usisite kupigia simu au mtumie sms na mwambie plans zako au kitu unachofanya kwa mda huo yaani muonyeshe kuwa upo nae mda wote.

Muonyeshe kuwa unampenda

Muonyeshe mpenzi wako jinsi gani unampenda na unamuhitaji kila mara. Usiogope kumwambia kila kitu kilichopo moyoni mwako, ukimwambia itawafanya wote mjisikie kila kitu kiko sawa. Kumwambia unapenda sana sio kitu cha aibu, Mwambie “Nakupendaa” Tena ukimwambia kabisa mbele yake uso kwa uso itamfanya ajisikie yuko na amani kuhusu swala la kuwa na mpenzi mwaminifu. Kuna njia nyingi za kumuonyesha kuwa unampenda, Mpe zawadi ndogo ndogo au ongea nae kuhusu mapenzi.





Fahamu mambo kuhusu mahusiano yake ya zaman
Watu wengine wanaumizwa na baadae wanakumbuka nini kilitokea kwao miaka mitano iliyopita. Mpenzi wako anaweza kuwa na wivu kwa sababu tu mahusiano yake ya zamani hayakua mazuri na yenye furaha. Je kama alidanganywa na kuachwa au mpenzi wake alitoka na tu mwingine? Kama hii ndio issue basi unatakiwa kulifahamu ilo na kumounyesha unampenda na ugundue kuwa anahitaji mda kuja kukuamini asilimia mia moja kuwa wewe ndie wa kweli.
Kama itasaidia maana kuna wapenzi wengine wana wivu hata ufanyeje.