JINSI YA KUACHA KUPOTEZA MUDA WAKO BILA SABABU ZA MSINGI.
Je wewe huwa unapoteza mda? Kukaa ukianalia movie au kuwa katika mitandao ya kijamii wakati unajua kuna kazi inakusubiri? Basii hapa nataka niongelee juu ya njia ambazo zinaweza kukusaidia uache kupoteza mda wako bila sababu.
Naenda moja kwa moja kwenye point maana hii ni tabia ambayo sema kweli wengi wetu tunashindwa kujirekebisha
Hatua ya kwanza
Kaa na urelax na baadae angalia kazi ambazo unatakiwa kufanya. Angalia vitu ambavyo unatakiwa kuvifanya na kuvimaliza na uangalie ni jinsi unaweza kuvifanya. Hata kama hii itakua ngumu kwa sababu ya vishawishi na vya kufanya vitu vingine lakini ukiwa unajua nini cha kufanya itakua rahisi kwako.
Tengeneza mpango wa kazi, ambazo unatakiwa kufanya, ukitengeneza mpango unafanya kazi zinakua rahisi kwako kwa kufanya kazi ambazo ulitakiwa kuzifanya. Bila kuwa na mpango mambo yako hayatakuendea sawa na utaendelea kupoteza mda kwa kufanya vitu ambavyo havina maana kwako. Nakwambia ukweli ni dakika 5 tu unazotumia kuapanga kazi ambazo zipo mbele yako ndani ya siku. Unaanza na kuyapa kipaumbele kazi ambazo unaona ni za muhimu sanaa.. Kwa kutengeneza ratiba ya kazi utakua na mafanikio mengi kuliko unaamka asubuhi wala hujui una kazi gani za kufanya ndani ya hiyo siku.
Fata mpango kazi wako. Watu mara nyingi wanaweza kutengeneza mpango kazi na ratiba vizuuri. Ila sasaaa ngoja kwenye kuifata ndipo kuna utata. Ukitaka kuacha kupoteza mda wako basi fata ratiba ya kazi zako uliyoitengeza mwenyewe. Baati nzuri unakua umeiandika mwenyewe. Yaani narudia tena Fata Ratiba uliyoitengeneza maana hiyo ndio muongozo wa kazi zako za kila siku. Hii iko hivi ratiba yako ulipanga saa sita unaenda kariakoo kuchukua mzigo na kuupeleka huko unakotakiwa kwenda na una uhakika kabisa utaenda, ila cjui kwa nini unaacha kwenda kariakoo hiyo saa sita unasema kwanza uende hospitali kumuona mgonjwa. Jamani ratiba ya kwenda kumuona mgonjwa si ilikua jioni?
Anza kufanya kazi, Usiache kufanya kazi mpaka uimalize. Fanya kitu kimoja kwa wakati mmoja na ukimalize, kama ukijisikia umechoka, basi chukua glass ya maji, au sikiliza mziki (ila sio ofisini) lakini endelea kufanya kazi ambayo iko mbele yako. Mpaka uimalize
Acha kuvutwa na vishawishi. Ehm tuangalie hii, watu wengine wako huru sana na vishawishi kuliko wengine. Hivi umeshawahi kujikuta unaanza kufanya kazi iliyopanga alafu unatumiwa text na mtu, tayari unaanza kuchat nae huku unafanya kazi, badala ya kumwambia uko kazini?
Hii inaonyesha unakaribisha vishawishi kwenye maisha yako kama sumaku. Mfano mzuri whats app. Tuseme Amina kakutumia text ukajibu, David kaona upo online anajua hauko bize anakutumia text unaijibu then tayari unaanza kuchati nao huku unafanya kazi.
Hauko peke yako, wapo watu weng sana na njia rahisi ya kuepukana na hii tabia ni kuwa makini na kazi zako unazotakiwa kuzifanya. Kama unaona simu inakuchanganya iweke silence ukiwa kazini, na kama mtu akikutumia text ambayo sio ya lazima kujibu muache atajua uko bize na kazi.