




SERIKALI ya Iraq leo imekabidhi mwili wa Izzat Ibrahim al-Douri (72) kwa wizara ya Afya ya Iraq kwa uchunguzi zaidi.
Mwili huo ulitembezwa katika gari kwenye mitaa mbalimbali na kuonyeshwa moja kwa moja na Televisioni ya Irag.
Izzat alikuwa mfuasi wa Saddam Hussein na alikuwa Kamanda wa Kundi la ISIS na aliuawa katika mapigano na majeshi ya serikali kwenye Mji wa Tikrit, siku ya Ijumaa.
Marehemu Izzat ameacha watoto sita ambao ni Ibrahim al-Douri, Abla al-Douri, Ahmed al-Douri, Hamraa' al-Douri, Ali al-Douri, Houzan al-Douri .