AJALI YA BASI NA LORI YAUA 10 SHINYANGA





Ajali za barabarani zimeendelea kujitokeza nchini Tanzania ambapo leo majira ya saa tisa kasorobo alasiri watu 10 wamefariki dunia na wengine 50 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Unique Express lenye namba za usajili T148 kugongana na lori aina ya scania lenye namba za usajili T207 BSA na tela lenye namba za usajili T635 AJT mali ya kampuni ya Coca Cola katika barabara ya Tinde Shinyanga eneo la kijiji cha Ibingo kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog




Maafisa wa polisi na wataalam wa afya kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la ajali.Mashuhuda wa tukio wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa lori alikuwa anaendesha gari akiwa katikati ya barabara huku dereva wa basi akiwa katika mwendo kasi hali ambayo katika kukwepa basi hilo aligonga tela la lori kisha kupinduka.





Wataalam awa afya wakiangalia miili iliyonasa kwenye basi


Basi likiwa limepinduka



Tela la lori la kampuni ya Coca cola lililokuwa linaelekea Shinyanga



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyekuwa eneo la tukio alisema watu 10 wamepoteza maisha katika ajali hiyo kati yao 9 walifariki dunia papo hapo huku majeruhi 50 wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja wa kiume wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.






Miili ya marehemu ikiwa imenasa kwenye basi





Kulia ni Kelvin Moshi mkazi wa Tanga aliyenusurika ifo katika ajali hiyo,aliyekuwa anasafiri kutoka Mwanza kwenda Tabora amesema dereva wa basi alikuwa katika mwendo kasi hali ambayo ilimfanya basi limshinde na kugongana na lori hilo.




Miili ya marehemu ikiwekwa kwenye lori baada ya kutolewa kwenye basi




Basi la Unique Express baada ya kuinuliwa na kuondoa miili ya watu watatu waliokuwa wamenasa kwenye basi




Maafisa wa polisi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio





Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio,Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog