







-Atua Las Vegas kwa basi sambamba na wapambe wake akitokea Los Angeles alipokuwa akijifua
-Ataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi
-Akataa sherehe rasmi za mapokezi yake, kuandaa sherehe yake leo kwenye hoteli
BONDIA mahiri kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao (36) jana usiku ametua jijini Las Vegas tayari kwa pambano lake la kihistoria dhidi ya Floyd Mayweather. Pambano hilo litapigwa Mei 2, mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand uliopo Las Vegas, Marekani.
Pacquiao ametua kwa basi akiambatana na wapambe wake akitokea Los Angeles umbali wa maili 270 alipokuwa akijifua.
Bondia huyo amesema anataka kumchakaza Mayweather katika kila raundi na hategemi sana kumchapa kwa knock-out (KO).
Manny pia amekataa sherehe rasmi za mapokezi yake na kusema kuwa ataandaa sherehe yake leo kwenye hoteli aliyofikia ya Mandalay Bay.