Bima Yamuokoa Mwanamuziki Diamond




Nyota wa muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’,

Nyota wa muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake uliodondoka.

Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.

“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka wakati huo nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu mpya, Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa ningekuwa kwenye hali gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alisema Diamond

Huku akiwataka watanzania wakate bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa na majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.