STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amefunguka kuwa tayari amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari' na anatarajia kupata mtoto wa kike mwaka huu.

Katika mahojiano hayo…

STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amefunguka kuwa tayari amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari' na anatarajia kupata mtoto wa kike mwaka huu.

Katika mahojiano hayo ambayo Diamond ameambatana na mpenzi wake huyo, ameongeza kuwa anatarajia kuingia katika ndoa mwaka huu.
Kwa upande wa Zari yeye amefunguka kuwa bado hajajua jina watakalompa mtoto wao wa kike anayetarajiwa kuzaliwa mwaka huu ila watampatia jina zuri la Kiislam na lenye mvuto