ZARI AZUA KIZAAZAA MSIBANI



Dustan Shekidele, Morogoro
Kazi ipo! Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ juzikati alizua kizaazaa kisa ujauzito alipohudhuria kwenye msiba wa aliyekuwa bosi wa Tip Top Connection, Abdul Taletale ‘Abdul Bonge’ aliyefariki dunia ghafla wikiendi iliyopita.

Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari akifichwa na bodigadi wake.

Tukio hilo la Zari lilichukua nafasi katika Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Matombo mkoani hapa ambapo mastaa kibao walisafiri kutoka Dar kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo.

ILIKUWAJE?
Awali, katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa mapema Jumanne wiki hii, Zari na Diamond, wakiwa wameongozana na wapambe wao walifika eneo la msiba ambapo kwa taratibu za Kiislam, wanawake hawachanganyiki na wanaume hivyo Zari akachukuliwa kwenda upande mwingine huku Diamond akielekea upande wa wanaume.

HALI YA HEWA YABADILIKA
Mara baada ya mastaa hao kutinga eneo hilo, umati mkubwa uliokuwa msibani hapo ulianza kuwazingira huku kila mmoja akitaka kuwaona.Akiingizwa garini.

ZARI AIBUA KIZAAZAA
Akiwa upande wa wanawake wenzake, Zari alijikuta akizungukwa na baadhi ya watu walionekana wazi kumchunguza kuanzia miguuni hadi kichwani ikidaiwa kuwa, walikuwa wakicheki kama kweli ana mimba ya Diamond.

“Mwee, huyu ndiye Zari wa Diamond! Hivi mimba anayo kweli au ndiyo haya mambo ya mastaa wetu, mhh lakini kweli kitumbo kama kimetuna vile,” alisikika akisema mmoja wa wanawake hao.Uwepo wa mwanadada huyo uliwafanya wengi kusahau ishu ya msiba na kujikuta wakipigana vikumbo kumshangaa Zari ambaye muda mwingi alikuwa akijificha.

Kutokana na mazingira ya watu kukanyagana kutaka kumuona staa huyo, mrembo aliyefahamika kwa jina la Jestina George aligeuka kuwa bodigadi wake ili kumuepushia usumbufu ambapo alifanya kazi ya kumlinda.

PAPARAZI AZUIWA KUMPIGA PICHA
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la msiba kwa lengo la kupata picha za kumbukumbu kwamba Zari aliwahi kufika eneo hilo, alikumbana na wakati mgumu baada ya Jestina kumpiga mkwara asijaribu kupiga picha.
“Weee, ukijaribu kupiga picha tunakorofishana, mwenyewe hataki kupiga picha, kama vipi nenda kamuombe ruhusa Diamond,” alisema Jestina huku akimficha Zari.Diamond akiimalisha usalama kwa mpenzi wake.

WATU WAANZA ZOGO
Kufuatia kitendo cha Jestina kumzuia mwandishi wetu kupiga picha, zogo lilianza eneo hilo huku baadhi ya watu wakihoji sababu za Zari kufichwa.“Au ni hiyo mimba yake ndiyo maana hamtaki apigwe picha? Acheni hizo bwana,” alisikika akiwaka kijana mmoja.

PAPARAZI AMFUATA DIAMOND
Baada ya paparazi kupigwa mkwara asipige picha alilazimika kwenda kumtafuta Diamond ili ampe ruhusa ya kwenda kumfotoa Zari lakini staa huyo naye alikataa na kueleza kuwa, kama anataka kufanya hivyo akachukue ruhusa kutoka kwa meneja wake.

Meneje huyo wa Diamond aliyefahamika kwa jina moja la Salam alipofuatwa alimruhusu paparazi kufanya kazi yake lakini aliporudi nyumbani palipokuwa na msiba kwa nia ya kumfotoa Zari, hali ilikuwa ileile hivyo kumsubiria mpaka Diamond alipotoka makaburini na alipofika kwenye gari lao, Zari alitolewa kwa kufichwa na Jestina kiasi cha kuwepo ugumu kupata sura yake.

ZARI AINGIA KWENYE GARI FASTA
Huku watu wakimfuata kwa nyuma, Jestina alimchukua Zari na kumficha kwapani kisha kumkimbizia kwenye gari tayari kwa kuondoka eneo hilo.

DIAMOND NAYE APATA WAKATI MGUMU
Wakati Diamond akirejea kutoka makaburini, alijikuta akizingirwa na baadhi ya vijana ambao wengi wao hawajawahi kumuona ‘live’ hivyo kumpa wakati mgumu.Hata hivyo, ili kuwafurahisha, vijana hao walipata fursa ya kupiga naye stori mbili-tatu kabla ya kuondoka eneo hilo na kuacha umati ukiwasindikiza kwa macho.