INAKUHUSU:Je wajua kwanini watu hushindwa kwanza ndipo wanafaulu maishani?



Kila mtu anajua kushindwa au kufeli ni kubaya sana. Hakuna siri kwamba kila unayemwona amefanikiwa sasa kuna sehemu fulani kwenye maisha yake alishawahi kushindwa au kufeli.



Kuna wengine wakishindwa mara moja hukata tamaa na wengine huinuka tena na kuendelea inategemeana na mtizamo wa huyo mtu kufikia mafanikio. Je unapambana vipi katika hali ya kushindwa? Unachotakiwa kufanya ni kubadilisha mtazamo wako na uelewa wako wa mambo, hapa nakupa mambo matano kwanini kushindwa sio kubaya kama unavyofikiri;

1. Kufeli au Kushindwa ni vitu unavyoviondoa njiani

Unapoweka malengo makubwa na uwezekano wa kushindwa pia upo. Uzoefu huu ni wa kawaida sana na upo kwenye maisha ya kila siku, na hasa unapokuwa mdogo kuna vitu vingi unawaza na kuona namna ambavyo utakuwa hapo baadaye lakini unaweza kujikuta hata robo ya kile ulichokiwaza bado haujafika mpaka sasa. Mwisho wa siku wewe ni binadamu wa kawaida ambaye huwa namna ambavyo unataka uwe kwa kupitia changamoto za kila siku ambazo unashindwa na kujaribu tena.

2. Unajifunza kitu kupitia kushindwa

Inawezekana umepoteza fedha kwa sababu biashara yako ilishindwa au kufa kabisa. Hii inatokea labda ulifanya makosa makubwa au kukosa umakini fulani ukakupelekea kuua biashara hiyo, lakini kuna kitu umejifunza kama umegundua makosa yako. Hapa unapata uzoefu wa kukufundisha ambao hupaswi kufanya siku nyingine, hivyo inakupa nyenzo ya kuendelea mbele wakati mwingine.

3. Makosa yanakusaidia kutengeneza Historia yako

Je unaweza kuwa na historia ambayo inaonyesha mafanikio mwanzo mwisho? Kinachowavutia watu wengi ni zile changamoto ulizopitia mpaka ukaweza kufanikiwa. Wewe kama umefanikiwa na haujapitia changamoto ambayo uko tayari kuiweka hadharani, watu watakuwa na mashaka na mafanikio yako, unaonyesha vitu ambavyo si kweli. Sio kila mtu anaweza kuhusianisha utajiri na mafanikio, lakini wengi huoanisha kupitia changamoto ulizopatakufika hapo ulipo.

4. Makosa au Kushindwa kunakujengea msingi Imara

Makosa na kushindwa ni kikumbushio kizuri kwamba sisi ni binadamu. Unapokuwa umezoea kufanikiwa kila siku inaweza kukufanya ukawa mzembe na kubweteka. Badala ya kuangalia ubaya wa kushindwa bali unapaswa kuangalia fursa na mlango mwingine wa kutoka hapo ulipo ili uweze kufanya vizuri zaidi.

5. Unapata fursa ya kufanya vizuri zaidi

Kwenye mahojiano na mjasiriamali mmoja anasema kwamba wafanyabiashara ambayo walishawahi kushindwa na wakainuka tena huwa wanapata fursa sawa kwa wawekezaji. Hivyo unavyojitahidi na kuweka juhudi kubwa inawezekana ulishindwa kijasiri na mwishowe kwamba kila biashara mia moja zinazoanzishwa tisini hushindwa ina maana biashara kumi huweza kuendelea. Si kila wakati mambo yatakwenda kwa staili yako unayoitaka kitu cha muhimu ni kuweka juhudi na uwe mtu mwenye kuona malengo yanatimia mpaka uone mafanikio unayohitaji. Kumbuka si rahisi na wala haitakuwa rahisi, ila atakayevumilia na kuweka juhudi ndiye atakayefanikiwa vizuri kufikia malengo yake.