Adam Mchomvu kwenda China kusomea ubunifu wa mavazi



Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, Adam Mchomvu ni mmoja kati ya wabunifu wa mavazi wachanga watakaopelekwa na THT nchini China kujifunza zaidi fani hiyo.
Akiongea kweye 255 ya XXL, mwanzilishi wa kituo hicho na mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amedai kuwa Adam ni designer mzuri anayetakiwa kupewa elimu ya umaliziaji ili aive.
Ruge amemwelezea Mchomvu kama mtu mwenye kipaji na mwenye ubunifu mkubwa.




Hivi karibuni kituo cha THT kilianza kujihusisha pia na masuala ya ubunifu wa mitindo.