DHAMBI YA PASAKA HATARI SANA
Issa Mnally na Richard Bukos
AMA KWELI duniani kuna mambo! Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mtu yeye alijikuta akiiserebukia kwa fumanizi gesti, tena akiwa na mume wa mtu!
Mwanamke aliyefumaniwa gesti akijivinjari na mume wa mtu.
Tukio hilo lilijiri Alhamisi Kuu maeneo Buza jijini Dar, mishale ya saa 7:00 usiku huku jamii ikiwa katika harakati za kununua hiki na kile kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa duniani kote jana huku leo ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka.
...akivaa nguo zake ili wapelekwe kituo cha polisi.
Katika fumanizi hilo, timbwili la aina yake liliibuka baada ya mwanamke huyo mwenye mwili mkubwa, kuponyoka mikononi mwa mke aliyemnasa na kutoka nduki nje akiwa mtupu bila kujali hali hiyo.
...akichukua vitu vyake na kupakia kwenye mkoba tayari kwa kupelekwa kituo cha polisi.
MADAI YA AWALI
Awali, ilidaiwa kuwa mume huyo wa mtu aliyefahamika kwa jina la baba Somoe, mkazi wa Kongowe (nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam) alimchepuka mke wake (mama Somoe) na kuanzisha uhusiano na mwanamke huyo.
...akijitetea kwa mgoni wake wakati wakipelekwa kituo cha polisi.
MKE ATILIA SHAKA, AFUATILIA
Chanzo kikazidi kudai kwamba mkewe huyo alianza kutilia shaka mwenendo wa mumewe kutokana na kubadili tabia, hasa za kuwa beneti na simu hivyo alianza kumfuatilia kwa karibu.
“Katika kumfuatilia, siku moja akabaini meseji. Akamuuliza mumewe kuhusu meseji hiyo naye akawayawaya bila kuwa na majibu sahihi,” kilisema chanzo hicho.
MKE AWEKA MASHARTI MAGUMU
Habari zaidi zilisema kuwa kutokana na ukweli kwamba, ndani ya nyumba yao, mama Somoe ndiyo kajaliwa uwezo wa kumiliki fedha, alimpa masharti mumewe kwamba achague mawili, watengane na aondoke na begi lake la nguo au atoe ushirikiano, ‘mwizi’ huyo anaswe.
“Mume akasema cha kufia! Akakubali kutoa ushirikiano ili mchepuko wake afumaniwe,” kilidai chanzo chetu.
OFM WALIFIKAJE ENEO LA TUKIO?
Ni kawaida kwa makamanda wa Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kinachomilikiwa na Global Publishers kuzunguka katika viunga vya Jiji la Dar ili kusaka matukio, ndipo katika harakati hizo, wakajikuta wameibukia mtaa wenye sekeseke hilo la aina yake.
OFM: “Kuna nini hapa?”
Shuhuda: “Kuna fumanizi. Kuna mke wa mtu amefumaniwa na mume wa mtu gesti, inasemekana ni mtego wa mke.
KUTOKA NDANI
Kelele za ‘huyo…huyo! Jamani niacheni…hamna… umezoea leo nimekunasa, loo! Hata aibu huna…kwani nimekufanya nini?’ zilisikika kutoka ndani.
OFM walitinga hadi ndani ya gesti hiyo na kukuta timbwili la aina yake ambapo mshikemshike nguo kuchanika ndiyo ilikuwa habari yenyewe.
Baada ya kubaini anapigwa picha na OFM, mwanamke huyo alitoka baruti akikimbizwa kwa nyuma na mwanamke aliyedai amemfumania sanjari na polisi huku picha zikiendelea kupigwa.
POLISI WAMDAKA
Nje, polisi walifanikiwa kumdaka na kumpiga pingu yeye na mwanaume aliyekuwa naye, yaani baba Somoe
MKE AZUNGUMZA NA OFM
Akizungumza na OFM baada ya utulivu kurejea huku watuhumiwa wakiwa anda aresti (chini ya ulinzi), mama Somoe alisema:
“Nimeamua kufanya hivi baada ya kuzifuma meseji nyingi za kimapenzi katika simu ya mume wangu. Nilipombana alikiri kuwa na mchepuko nje ya ndoa lakini aliniomba msamaha.
“Hata hivyo, pamoja na kuniomba msamaha bado mwenendo wake haukuwa mzuri, alikuwa bize sana na simu yake. Sasa jana (Jumatano iliyopita) alipokwenda kuoga ikaingia meseji kwenye simu yake, akiambiwa tayari ameshawekewa chumba kwenye gesti hii.
“Meseji hiyo ilisema hivi; kaka ulisema tukuwekee chumba chako kile cha mauaji lakini bahati mbaya kina mgeni tangu jana, tumekuwekea chumba namba A3. Mimi mhudumu hapa gesti...” (jina la gesti tunalihifadhi).
Mwanamke huyo alidai kuwa akiwa na kaka yake, baada ya kuwapata askari, walikwenda kugonga kwenye chumba hicho, walipofungua yeye aliangua kilio baada ya kumkuta mumewe akiwa na mchepuko huo kitandani.
KUHUSU MTEGO
Mama Somoe alisema hajui lolote kuhusu yeye kumuwekea mtego mwanamke huyo bali anachojua ni SMS za mtu wa gesti ndiyo ziliibua mambo.