BALAA LA MGOMO WA MADEREVA DAR NI HATARI TUPU




Hii picha ni mabasi yaendayo mikoani yakiwa ndani ya stendi ya Ubungo yamegoma kufanya kazi yoyote



Haya ni baadhi matairi ya magari yalichomwa na baadhi wananchi maeneo ya stendi kuu ya Ubungo jijini Dar ila Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha wananchi hao. Lakini baadhi ya Wananchi hawakukubali hilo nao wakaanza kushika mawe na kuwarushia Polisi, ikawa ni mawe VS Mabomu. Haya yote chanzo ni mgomo wa Madereva ulioanza leo nchi nzima.





Wananchi wakitumia lori kusafiri


Katika eneo la stendi ya Ubungo polisi imewalazimu kutumia mabomu ya machozi kusambaratisha abiria waliokuwa wamekusanyika eneo hilo wakitaka kujua hatma ya usafiri wao kwenda mikoani.


Kuna taarifa kuwa zaidi ya mabasi 10 kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa yamekwama wilayani Kibaha wakihofia vurugu kutokana na mgomo unaoendelea.



Umati wa watu eneo la Ubungo stendi, uliosababisha Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya







Umati wa watu eneo la Ubungo stendi, uliosababisha Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya





Hii picha ni mabasi yaendayo mikoani yakiwa ndani ya stendi ya Ubungo yamegoma kufanya kazi yoyote










Mabasi yaendayo mikoani yakiwa Stendi ya Ubungo yamepaki.

Wasafiri wakiwa hawajui hatma ya safari yao eneo la Ubungo.

Hali halisi ya Ubungo ilivyokuwa asubuhi leo.

Muonekano wa eneo la Ubungo-Darajani hali ilivyokuwa.

Kituo cha daladala cha Shekilango hali ilivyokuwa.

Umati mkubwa wa watu ukimshudia jamaa mmoja aliyekuwa akitoa ibada fupi ya kuombea nchi kuhusiana na mgomo wa madereva ambao ni wa nchi nzima eneo la Ubungo.

Usafiri wa bodaboda ukionekana kufanya kazi bila kugoma.

Madereva wa Bajaj nao wakipakia abiria
Abiria wakitafakari kuhusu safari yao.
Madereva wa mabasi ya mikoani na daladala wa jijini Dar es salaam leo wamefanya mgomo kupinga agizo la Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) lililowataka kwenda kusoma katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Mwandishi wetu amezunguka maeneo tofauti tofauti jijini Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani pamoja na daladala za maeneo tofauti ya Jiji la Dar.

Mwandishi wetu pia aliweza kufika eneo la Stendi ya Ubongo na kujionea hali ilivyokuwa asubuhi na kuzungumza na baadhi ya madereva ambao walikuwa na kauli tofautitofati kuhusiana na mgomo huo.

Mmoja wa madereva ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdallah Shalon anayefanya kazi zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma, alisema kuwa sababu kubwa ya kutokufanya shughuli zake ni kutokana na kikao ambacho walipanga kukifanya leo kujadili agizo la Sumatra lililowataka waende shule kusoma.

Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Khamis anayefanya shughuli zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam alisema sababu iliyomfanya agome ni kupinga sheria mpya ya Sumatra iliyopitishwa na jeshi la polisi kuwataka madereva wote wa abiria (Pasangers Services Vehicle) kwenda kusoma kozi ya miezi miwili kwa gharama ya shilingi laki tano.


Khamis alisema sheria hiyo inawabana sana madereva kwani moja kati ya vipengele vya sheria hiyo imeeleza kuwa, dereva yeyote atakayekamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi hakuna faini yoyote bali unapelekwa mahabusu kwa muda wa siku kumi na nne baada ya kumaliza siku hizo, anapelekwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.



“Hii sheria inatubana sana, mtu ukihitaji kubadilisha leseni yako ikipitwa na muda unatakiwa kurudia tena kwenda kusoma darasani kwa muda wa wiki mbili kwa ada isiyopungua laki tano na kuendelea kitu ambacho kinatuumiza sisi madereva,” alisema Khamisi